Zaburi 139:19-22
Zaburi 139:19-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu! Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu! Wanasema vibaya juu yako; wanasema maovu juu ya jina lako! Ee Mwenyezi-Mungu, nawachukia wanaokuchukia; nawadharau sana wale wanaokuasi! Maadui zako ni maadui zangu; ninawachukia kabisakabisa.
Zaburi 139:19-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu; Wale wanaokusema kwa ubaya, na kutenda maovu juu ya jina lako bure. Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiudhike nao watu wanaokuasi? Nawachukia kwa upepo wa chuki, Wamekuwa adui kwangu.
Zaburi 139:19-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, laiti ungewafisha waovu! Enyi watu wa damu, ondokeni kwangu; Kwa maana wakuasi kwa ubaya, Adui zako wakutaja jina lako bure. Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia? Nisikirihike nao wakuasio? Nawachukia kwa ukomo wa chuki, Wamekuwa adui kwangu.
Zaburi 139:19-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu! Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, adui zako wanatumia vibaya jina lako. Ee BWANA, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako? Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, ninawahesabu ni adui zangu.