Zaburi 139:1-3
Zaburi 139:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani. Nikiketi au nikisimama, wewe wajua; wajua kutoka mbali kila kitu ninachofikiria. Watambua nikienda au nikipumzika; wewe wazijua shughuli zangu zote.
Shirikisha
Soma Zaburi 139Zaburi 139:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kusimama kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.
Shirikisha
Soma Zaburi 139