Zaburi 133:1-3
Zaburi 133:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri yatiririkayo kichwani, mpaka kwenye ndevu zake Aroni, mpaka upindoni mwa vazi lake shingoni. Ni kama umande wa mlima Hermoni, uangukao juu ya vilima vya Siyoni! Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake, kuwapa uhai usio na mwisho.
Zaburi 133:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
Zaburi 133:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
Zaburi 133:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Haruni, hadi kwenye upindo wa mavazi yake. Ni kama umande wa Hermoni ukianguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka yake, naam, uzima hata milele.