Zaburi 132:1-12
Zaburi 132:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, mkumbuke Daudi, kumbuka taabu zote alizopata. Ukumbuke ahadi aliyokupa, ee Mwenyezi-Mungu, kiapo alichokuapia, ewe Mwenye Nguvu wa Yakobo: “Sitaingia ndani ya nyumba yangu, wala kulala kitandani mwangu; sitakubali kulala usingizi, wala kusinzia; mpaka nikupatie wewe Mwenyezi-Mungu mahali pa kukaa, makao yako, ewe Mwenye Nguvu wa Yakobo!” Huko Efratha tulisikia habari za sanduku la agano, tukalikuta katika mashamba ya Yearimu. “Haya! Twende nyumbani kwa Mungu, tuabudu mbele ya kiti chake cha enzi!” Inuka ee Mwenyezi-Mungu, nenda kwenye maskani yako; inuka pamoja na sanduku la agano la uwezo wako! Makuhani wako wawe waadilifu daima; na waaminifu wako wapige vigelegele vya furaha! Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, usimkatae huyo mfalme uliyemweka wakfu. Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi kiapo thabiti, kiapo ambacho hatakibatilisha: “Nitamtawaza mmoja wa wazawa wako mwenyewe, kuwa mfalme baada yako. Watoto wako wakishika agano langu, na kuzingatia mafundisho nitakayowapa, watoto wao pia watakuwa wafalme kama wewe.”
Zaburi 132:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika. Vile alivyomwapia BWANA, Akaweka nadhiri kwa ewe Mwenye nguvu wa Yakobo. “Sitaingia nyumbani mwangu, Wala sitalala kitandani mwangu; Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia; Hadi nitakapompatia BWANA mahali, Na Mwenye nguvu wa Yakobo maskani”. Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika shamba la Yearimu tuliiona. Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. Ee BWANA, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie. Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, Usiurudishe nyuma uso wa masihi wako. BWANA amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalivunja, Mmoja wa wazawa wako mwenyewe Nitawaweka katika kiti chako cha enzi. Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele.
Zaburi 132:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika. Ndiye aliyemwapia BWANA, Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo. Sitaingia hemani mwa nyumba yangu, Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu; Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia; Hata nitakapompatia BWANA mahali, Na Shujaa wa Yakobo maskani. Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika konde la Yearimu tuliiona. Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. Ee BWANA, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie. Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, Usiurudishe nyuma uso wa masihi wako. BWANA amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa mwili wako Nitawaweka katika kiti chako cha enzi. Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele.
Zaburi 132:1-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili. Aliapa kiapo kwa BWANA na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: “Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu: sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia, hadi nitakapompatia BWANA mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” Tulisikia habari hii huko Efrata, tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara: “Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; inuka, Ee BWANA, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako. BWANA alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe kwenye kiti chako cha ufalme, kama wanao watashika agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watakalia kiti chako cha ufalme milele na milele.”