Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 13:1-2 - Compare All Versions

Zaburi 13:1-2 BHN (Biblia Habari Njema)

Mpaka lini ee Mwenyezi-Mungu, utanisahau? Je, utanisahau mpaka milele? Mpaka lini utanificha uso wako? Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini, na sikitiko moyoni siku hata siku? Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu?

Shirikisha
Zaburi 13 BHN

Zaburi 13:1-2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Ee BWANA, hata lini utanisahau, hata milele? Hata lini utanificha uso wako? Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?

Shirikisha
Zaburi 13 SUV

Zaburi 13:1-2 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele? Hadi lini utanificha uso wako? Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?

Shirikisha
Zaburi 13 SRUV

Zaburi 13:1-2 NEN (Neno)

Hadi lini, Ee BWANA? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako hadi lini? Nitapambana na mawazo yangu hadi lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda hadi lini?

Shirikisha
Zaburi 13 NEN