Zaburi 121:1-5
Zaburi 121:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia. Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii. Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali. Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga.
Zaburi 121:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu hutoka kwa BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. Hatauacha mguu wako usogezwe; Akulindaye hatasinzia; Naam, hatasinzia wala hatalala, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.
Zaburi 121:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
Zaburi 121:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nayainua macho yangu natazama milima: msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu hutoka kwa BWANA, Muumba wa mbingu na dunia. Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. BWANA anakulinda, BWANA ni uvuli wako mkono wako wa kuume