Zaburi 116:3-5
Zaburi 116:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Hatari ya kifo ilinizunguka, vitisho vya kaburi vilinivamia; nilijawa na mahangaiko na majonzi. Kisha nikamlilia Mwenyezi-Mungu: “Ee Mwenyezi-Mungu, tafadhali unisalimishe!” Mwenyezi-Mungu amejaa wema na uaminifu; Mungu wetu ni mwenye huruma.
Shirikisha
Soma Zaburi 116Zaburi 116:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Nilipata dhiki na mateso; Nikaliitia jina la BWANA. Ee BWANA, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. BWANA ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
Shirikisha
Soma Zaburi 116Zaburi 116:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la BWANA. Ee BWANA, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. BWANA ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
Shirikisha
Soma Zaburi 116