Zaburi 116:1-9
Zaburi 116:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Nampenda Mwenyezi-Mungu, kwa maana anisikia, maana amesikia kilio cha ombi langu. Yeye amenitegea sikio, hivyo nitamwomba muda wote niishio. Hatari ya kifo ilinizunguka, vitisho vya kaburi vilinivamia; nilijawa na mahangaiko na majonzi. Kisha nikamlilia Mwenyezi-Mungu: “Ee Mwenyezi-Mungu, tafadhali unisalimishe!” Mwenyezi-Mungu amejaa wema na uaminifu; Mungu wetu ni mwenye huruma. Mwenyezi-Mungu huwalinda wanyofu; nilipokuwa nimekandamizwa aliniokoa. Uwe na utulivu mkuu, ee nafsi yangu, maana Mwenyezi-Mungu amenitendea mema. Ameniokoa kifoni na kufuta machozi yangu; akanilinda nisije nikaanguka. Nitatembea mbele yake Mwenyezi-Mungu, katika nchi ya watu walio hai.
Zaburi 116:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Nilipata dhiki na mateso; Nikaliitia jina la BWANA. Ee BWANA, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. BWANA ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. BWANA huwalinda wasio na hila; Nilidhilika, akaniokoa. Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu. Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka. Nitaenenda mbele za BWANA Katika nchi za walio hai.
Zaburi 116:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la BWANA. Ee BWANA, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. BWANA ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. BWANA huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa. Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu. Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka. Nitaenenda mbele za BWANA Katika nchi za walio hai.
Zaburi 116:1-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nampenda BWANA kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie. Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu. Kamba za mauti zilinizunguka, vitisho vya Kuzimu vilinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. Ndipo nikaliitia jina la BWANA: “Ee BWANA, niokoe!” BWANA ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma. BWANA huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa. Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa BWANA amekuwa mwema kwako. Kwa kuwa wewe, Ee BWANA, umeniokoa nafsi yangu na mauti, macho yangu kutokana na machozi, miguu yangu kutokana na kujikwaa, ili niweze kutembea mbele za BWANA, katika nchi ya walio hai.