Zaburi 112:1-9
Zaburi 112:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki. Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele. Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA. Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa. Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Zaburi 112:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake. Wazawa wake watakuwa wenye nguvu nchini; watoto wa wanyofu watapata baraka. Nyumbani kwake kutakuwa na mali nyingi; uadilifu wake wadumu milele. Mtu mwema huangaziwa mwanga gizani; mtu mwenye huruma, mpole na mwadilifu. Mtu mkarimu akopeshaye bila faida, hufanikiwa; mtu afanyaye shughuli zake kwa kutumia haki. Mwadilifu hatashindwa kamwe, huyo atakumbukwa milele. Hana haja ya kuogopa akipata habari mbaya; ana moyo thabiti na humtegemea Mwenyezi-Mungu. Yuko imara moyoni, wala hataogopa; naye atawaona maadui zake wanashindwa. Hutoa kwa ukarimu, huwapa maskini; uadilifu wake wadumu milele. Nguvu yake inatukuzwa kwa heshima.
Zaburi 112:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Wazawa wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yadumu milele. Nuru huwaangaza wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki. Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele. Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumainia BWANA. Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa. Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Zaburi 112:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki. Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele. Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA. Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa. Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Zaburi 112:1-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Msifuni BWANA. Heri mtu yule amchaye BWANA, mtu yule apendezwaye sana na amri zake. Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, haki yake hudumu milele. Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki. Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, anayefanya mambo yake kwa haki. Hakika hatatikisika kamwe, mtu mwenye haki atakumbukwa milele. Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea BWANA. Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake. Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; haki yake hudumu milele; pembe yake itatukuzwa kwa heshima.