Zaburi 112:1-5
Zaburi 112:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake. Wazawa wake watakuwa wenye nguvu nchini; watoto wa wanyofu watapata baraka. Nyumbani kwake kutakuwa na mali nyingi; uadilifu wake wadumu milele. Mtu mwema huangaziwa mwanga gizani; mtu mwenye huruma, mpole na mwadilifu. Mtu mkarimu akopeshaye bila faida, hufanikiwa; mtu afanyaye shughuli zake kwa kutumia haki.
Zaburi 112:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Wazawa wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yadumu milele. Nuru huwaangaza wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.
Zaburi 112:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.
Zaburi 112:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Msifuni BWANA. Heri mtu yule amchaye BWANA, mtu yule apendezwaye sana na amri zake. Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, haki yake hudumu milele. Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki. Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, anayefanya mambo yake kwa haki.