Zaburi 11:4-6
Zaburi 11:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu yumo katika hekalu lake takatifu; kiti cha enzi cha Mwenyezi-Mungu kiko mbinguni. Kwa macho yake huwachungulia wanadamu, na kujua kila kitu wanachofanya. Mwenyezi-Mungu huwapima waadilifu na waovu; huwachukia kabisa watu wakatili. Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberiti; upepo wa hari utakuwa ndio adhabu yao.
Zaburi 11:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu. BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu. Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.
Zaburi 11:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawajaribu wanadamu. BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu. Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa hari, Na viwe fungu la kikombe chao.
Zaburi 11:4-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; BWANA yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawachunguza. BWANA huwachunguza wenye haki, lakini nafsi yake inachukia waovu na wale wanaopenda mapigano. Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka; upepo wenye joto kali ndio fungu lao.