Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 107:1-9 - Compare All Versions

Zaburi 107:1-9 BHN (Biblia Habari Njema)

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele! Semeni hivyo, enyi mliokombolewa na Mwenyezi-Mungu, watu ambao aliwaokoa katika taabu, akawakusanyeni kutoka nchi za kigeni: Kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini. Baadhi walitangatanga katika jangwa tupu, wasiweze kufikia mji wa kukaa. Waliona njaa na kiu; wakavunjika moyo kabisa. Ndipo katika taabu yao wakamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akawaokoa katika mateso yao. Aliwaongoza katika njia iliyonyoka, mpaka wakaufikia mji wa kukaa. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa fadhili zake; kwa sababu ya maajabu aliyowatendea binadamu. Yeye huwatosheleza walio na kiu; na wenye njaa huwashibisha mema.

Shirikisha
Zaburi 107 BHN

Zaburi 107:1-9 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na waseme hivi waliokombolewa na BWANA, Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi. Akawakusanya kutoka nchi zote, Mashariki na magharibi, kaskazini na kusini. Walitangatanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa. Waliona njaa na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa. Na wamshukuru BWANA, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. Maana hushibisha nafsi yenye shauku, Na nafsi yenye njaa huijaza mema.

Shirikisha
Zaburi 107 SRUV

Zaburi 107:1-9 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na waseme hivi waliokombolewa na BWANA, Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi. Akawakusanya kutoka nchi zote, Mashariki na magharibi, kaskazini na kusini. Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa. Waliona njaa, waliona na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa. Na wamshukuru BWANA, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. Maana hushibisha nafsi yenye shauku, Na nafsi yenye njaa huijaza mema.

Shirikisha
Zaburi 107 SUV

Zaburi 107:1-9 NEN (Neno)

Mshukuruni BWANA, kwa kuwa yeye ni mwema, fadhili zake zadumu milele. Waliokombolewa wa BWANA na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui, wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini. Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi. Walikuwa na njaa na kiu, nafsi zao zikadhoofika. Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. Akawaongoza kwa njia iliyo sawa hadi mji ambao wangeweza kuishi. Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.

Shirikisha
Zaburi 107 NEN