Zaburi 106:13-18
Zaburi 106:13-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini mara walisahau matendo yake, wakaacha kutegemea shauri lake. Walijawa na tamaa kubwa kule jangwani, wakamjaribu Mungu kule nyikani. Naye akawapa kile walichoomba, lakini akapeleka maradhi mabaya kati yao. Kule kambini walimwonea wivu Mose, na Aroni mtumishi mtakatifu wa Mwenyezi-Mungu. Ndipo ardhi ikafunguka ikammeza Dathani, na kumzika Abiramu na kundi lake lote; moto ukawatokea wafuasi wao, ukawateketeza watu hao waovu.
Zaburi 106:13-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini punde wakayasahau matendo yake, Wakakosa kungojea ushauri wake. Bali walitamani sana nyikani, Wakamjaribu Mungu jangwani. Akawapa walichomwomba, Lakini akawatumia ugonjwa wa kuwakondesha. Wakamhusudu Musa kambini, Na Haruni, mtakatifu wa BWANA. Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu. Moto ukawaka katika mkutano wao, Miali yake ikawateketeza waovu.
Zaburi 106:13-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakayasahau matendo yake kwa haraka, Hawakulingojea shauri lake. Bali walitamani sana jangwani, Wakamjaribu Mungu nyikani. Akawapa walichomtaka, Akawakondesha roho zao. Wakamhusudu Musa matuoni, Na Haruni, mtakatifu wa BWANA. Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu. Moto ukawaka katika mkutano wao, Miali yake ikawateketeza wabaya.
Zaburi 106:13-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini walisahau upesi aliyowatendea, wala hawakungojea ushauri wake. Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani. Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha. Kambini walimwonea wivu Musa, na pia Haruni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa BWANA. Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, ikawazika Abiramu na kundi lake. Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, mwali wa moto uliwateketeza waovu.