Zaburi 106:1-5
Zaburi 106:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Haleluya! Msifuni Mwenyezi-Mungu! Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele! Ni nani awezaye kutaja matendo ya Mwenyezi-Mungu? Ni nani awezaye kumsifu kama anavyostahili? Heri wale wanaotekeleza haki, wanaotenda daima mambo yaliyo sawa. Unikumbuke ee Mwenyezi-Mungu unapowafadhili watu wako; unisaidie wakati unapowaokoa; ili niweze kuona fanaka ya wateule wako, nipate kufurahia furaha ya taifa lako, na kuona fahari pamoja na watu wako.
Zaburi 106:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA, Au kuzihubiri sifa zake zote? Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote. Ee BWANA, unikumbuke mimi, Kwa kibali ulicho nacho kwa watu wako. Unijie kwa wokovu wako, Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.
Zaburi 106:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA, Kuzihubiri sifa zake zote? Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote. Ee BWANA, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako, Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.
Zaburi 106:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Msifuni BWANA. Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya BWANA au kutangaza kikamilifu sifa zake? Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema. Ee BWANA, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa, ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, na kuungana na urithi wako katika kukusifu.