Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 104:1-35

Zaburi 104:1-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama. Umejivika nuru kama vazi; Umezitandika mbingu kama pazia; Na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo, Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali. Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele. Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima. Kwa kukemea kwako yakakimbia, Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi, Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni, Mpaka mahali ulipoyatengenezea. Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi. Hupeleka chemchemi katika mabonde; Zapita kati ya milima; Zamnywesha kila mnyama wa kondeni; Punda mwitu huzima kiu yao. Kandokando hukaa ndege wa angani; Kati ya matawi hutoa sauti zao. Huinywesha milima toka orofa zake; Nchi imeshiba mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake. Miti ya BWANA nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao, Na korongo, misunobari ni nyumba yake. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, Jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku, Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo, Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu. Jua lachomoza, wanakwenda zao, Na kujilaza mapangoni mwao. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, Na kwenye utumishi wake mpaka jioni. Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai vidogo kwa vikubwa. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, Waipeleka roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi. Utukufu wa BWANA na udumu milele; BWANA na ayafurahie matendo yake. Aitazama nchi, inatetemeka; Aigusa milima, inatoka moshi. Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai; Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia BWANA. Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Shirikisha
Soma Zaburi 104

Zaburi 104:1-35 Biblia Habari Njema (BHN)

Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu mno! Umejivika utukufu na fahari. Umejizungushia mwanga kama vazi, umezitandaza mbingu kama hema; umejenga makao yako juu ya maji ya mbingu. Umeyafanya mawingu kuwa gari lako; waruka juu ya mabawa ya upepo, waufanya upepo kuwa mjumbe wako, moto na miali yake kuwa watumishi wako. Dunia umeiweka imara juu ya misingi yake, ili isitikisike milele. Uliifunika dunia kwa bahari kama vazi, na maji yakaimeza milima mirefu. Ulipoyakaripia, maji yalikimbia, yaliposikia ngurumo yako yalitimka mbio. Yaliporomoka toka milimani hadi mabondeni, mpaka pale mahali ulipoyatengenezea. Uliyawekea hayo maji mipaka, yasije yakaifunika tena dunia. Umetokeza chemchemi mabondeni, na mikondo yake ipite kati ya vilima. Hizo zawapatia maji wanyama wote porini. Humo pundamwitu huzima kiu zao. Ndege hujenga viota vyao katika miti ya hapo, hutua katika matawi yake na kuimba. Toka juu angani wainyeshea milima mvua, nayo dunia waitosheleza kwa baraka yako. Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo, na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini: Divai ya kumchangamsha, mafuta ya zeituni ya kumfurahisha, na mkate wa kumpa nguvu. Miti mikubwa ya Mwenyezi-Mungu yapata maji ya kutosha; naam, mierezi ya Lebanoni aliyoiotesha. Humo, ndege hujenga viota vyao; korongo hufanya maskani yao katika misonobari. Milima mirefu ni makao ya mbuzimwitu; na pelele hupata maficho yao miambani. Umeuumba mwezi utupimie majira; jua nalo lajua wakati wa kutua. Waleta giza, usiku waingia; nao wanyama wote wa porini wanatoka: Wanasimba hunguruma wapate mawindo, humngojea Mungu awape chakula chao. Jua lichomozapo hurudi makwao, na kujipumzisha mapangoni mwao. Hapo naye binadamu huenda kwenye shughuli zake; na kufanya kazi zake mpaka jioni. Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako! Mbali kule iko bahari - kubwa na pana, ambamo kumejaa viumbe visivyohesabika, viumbe hai, vikubwa na vidogo. Ndimo zinamosafiri meli, na lile dude Lewiyathani uliloliumba licheze humo. Wote wanakungojea wewe, uwapatie chakula chao kwa wakati wake. Wanaokota chochote kile unachowapa; ukifumbua mkono wako wanashiba vinono. Ukiwapa kisogo, wanaogopa; ukiondoa pumzi yao, wanakufa, na kurudi mavumbini walimotoka. Ukiwapulizia pumzi yako, wanaishi tena; wewe waipa dunia sura mpya. Utukufu wa Mwenyezi-Mungu udumu milele; Mwenyezi-Mungu apendezwe na matendo yake mwenyewe. Huitazama dunia nayo hutetemeka, huigusa milima nayo hutoa moshi! Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu maisha yangu yote; nitamsifu Mungu wangu muda wote niishipo. Upendezwe, ee Mwenyezi-Mungu, na mawazo yangu haya; maana furaha yangu naipata kwako. Wenye dhambi waondolewe duniani, pasiwe na waovu wowote tena! Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Msifuni Mwenyezi-Mungu!

Shirikisha
Soma Zaburi 104

Zaburi 104:1-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na utukufu. Umejivika nuru kama vazi; Umezitandika mbingu kama pazia; Na kuziweka nguzo za ghorofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo, Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali. Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele. Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima. Kwa kukemea kwako yakakimbia, Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi, Yakapanda milima, yakateremka mabondeni, Mpaka mahali ulipoyatengenezea. Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi. Hupeleka chemchemi katika mabonde; Zapita kati ya milima; Zamnywesha kila mnyama wa porini; Kwayo punda mwitu huzima kiu yao. Kandokando hukaa ndege wa angani; Na kuimba wakiwa katika matawi. Huinywesha milima toka juu angani; Nchi umeitosheleza kwa mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake. Miti ya BWANA nayo imetoshelezwa maji, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Humo ndege hujenga viota vyao, Korongo, anayo makao katika misonobari. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio lao wibari. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, Jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku, Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. Wanasimba hunguruma wakitaka mawindo, Wakitafuta chakula chao kutoka kwa Mungu. Jua linapochomoza, wanakwenda zao, Na kujilaza mapangoni mwao. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, Na kwenye utumishi wake mpaka jioni. Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa viumbe wako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai wakubwa kwa wadogo. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo Lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, Waituma roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi. Utukufu wa BWANA na udumu milele; BWANA na ayafurahie matendo yake. Aitazamaye nchi, ikatetemeka; Aigusaye milima, ikatoka moshi. Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai; Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Maana furaha yangu hutoka kwa BWANA. Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Shirikisha
Soma Zaburi 104

Zaburi 104:1-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama. Umejivika nuru kama vazi; Umezitandika mbingu kama pazia; Na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo, Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali. Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele. Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima. Kwa kukemea kwako yakakimbia, Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi, Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni, Mpaka mahali ulipoyatengenezea. Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi. Hupeleka chemchemi katika mabonde; Zapita kati ya milima; Zamnywesha kila mnyama wa kondeni; Punda mwitu huzima kiu yao. Kandokando hukaa ndege wa angani; Kati ya matawi hutoa sauti zao. Huinywesha milima toka orofa zake; Nchi imeshiba mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake. Miti ya BWANA nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao, Na korongo, misunobari ni nyumba yake. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, Jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku, Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo, Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu. Jua lachomoza, wanakwenda zao, Na kujilaza mapangoni mwao. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, Na kwenye utumishi wake mpaka jioni. Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai vidogo kwa vikubwa. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, Waipeleka roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi. Utukufu wa BWANA na udumu milele; BWANA na ayafurahie matendo yake. Aitazama nchi, inatetemeka; Aigusa milima, inatoka moshi. Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai; Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia BWANA. Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Shirikisha
Soma Zaburi 104

Zaburi 104:1-35 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Ee BWANA Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. BWANA amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema, na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake la vita, na hupanda kwenye mabawa ya upepo. Huzifanya pepo kuwa wajumbe wake, na miali ya moto kuwa watumishi wake. Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa. Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima. Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka, yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia. Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena. Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima. Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao. Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, huimba katika matawi. Huinyeshea milima kutoka orofa zake, dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake. Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini: divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu. Miti ya BWANA inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Humo ndege hufanya viota vyao, korongo ana nyumba yake kwenye msunobari. Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu; majabali ni kimbilio la pelele. Mwezi hugawanya majira, na jua hutambua wakati wake wa kutua. Unaleta giza, kunakuwa usiku, wanyama wote wa mwituni huzurura. Simba hunguruma kwa mawindo yao, na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu. Jua huchomoza, nao huondoka, hurudi na kulala katika mapango yao. Kisha wanadamu wanaenda kazini zao, katika kazi zao hadi jioni. Ee BWANA, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako. Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake. Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. Wakati unawapa, wanakikusanya; unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema. Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini. Unapopeleka Roho wako, wanaumbwa, nawe huufanya upya uso wa dunia. Utukufu wa BWANA na udumu milele, BWANA na azifurahie kazi zake: yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, aigusaye milima, nayo ikatoa moshi. Nitamwimbia BWANA maisha yangu yote; nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi. Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, ninapofurahi katika BWANA. Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia na waovu wasiwepo tena.

Shirikisha
Soma Zaburi 104