Zaburi 101:1-4
Zaburi 101:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Utenzi wangu kuhusu uaminifu na haki; ninauimba kwa heshima yako, ee Mwenyezi-Mungu. Nitazingatia mwenendo usio na hatia. Je, utakuja kwangu lini? Nitaishi kwa unyofu nyumbani kwangu; sitavumilia kamwe upuuzi. Nayachukia matendo ya watu wapotovu, mambo yao hayataambatana nami. Upotovu wowote ule uwe mbali nami; sitahusika kabisa na uovu.
Zaburi 101:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Rehema na hukumu nitaziimba, Ee BWANA, nitakuimbia zaburi. Nitakuwa na mwenendo usio na hatia; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu. Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami. Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.
Zaburi 101:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Rehema na hukumu nitaziimba, Ee BWANA, nitakuimbia zaburi. Nitaiangalia njia ya unyofu; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu. Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami. Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.
Zaburi 101:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nitaimba kuhusu upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee BWANA, nitaimba sifa. Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama. Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; hawatashikamana nami. Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; nitajitenga na kila ubaya.