Zaburi 100:1-3
Zaburi 100:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote! Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe! Jueni kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu. Yeye ndiye aliyetuumba, nasi ni mali yake; sisi ni watu wake, ni kondoo wa malisho yake.
Zaburi 100:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mshangilieni BWANA, enyi nchi zote; Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake mkiimba; Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
Zaburi 100:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote; Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba; Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
Zaburi 100:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mpigieni BWANA kelele za shangwe, dunia yote. Mwabuduni BWANA kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake.