Zaburi 10:14-15
Zaburi 10:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wewe wawaona wenye dhiki na shida; nawe daima uko tayari kuwasaidia. Mnyonge anakutegemea wewe, ee Mungu, wewe umekuwa daima msaada wa yatima. Uzivunje nguvu za mtu mwovu; ukomeshe uovu wake wote, usiwepo tena.
Zaburi 10:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima. Uuvunje mkono wa mdhalimu, Na mwovu, uipatilize dhuluma yake, hadi usiione.
Zaburi 10:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima. Uuvunje mkono wake mdhalimu, Na mbaya, uipatilize dhuluma yake, hata usiione.
Zaburi 10:14-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima. Vunja mkono wa mtu mbaya na mwovu; mwite mtu mbaya atoe hesabu ya uovu wake ambao usingejulikana vinginevyo.