Methali 9:7-10
Methali 9:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi, amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa. Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia; mwonye mwenye hekima naye atakupenda. Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili.
Methali 9:7-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu; Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
Methali 9:7-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu; Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
Methali 9:7-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Yeyote anayemkosoa mwenye dhihaka hukaribisha matusi; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi. Usimkemee mwenye dhihaka, la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda. Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika. “Kumcha BWANA ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.