Methali 8:1-11
Methali 8:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikilizeni! Hekima anaita! Busara anapaza sauti yake! Juu penye mwinuko karibu na njia, katika njia panda ndipo alipojiweka. Karibu na malango ya kuingilia mjini, mahali wanapoingia watu anaita kwa sauti: “Enyi watu wote, nawaita nyinyi! Wito wangu ni kwa ajili ya binadamu. Enyi wajinga, jifunzeni kuwa na akili; sikilizeni kwa makini enyi wapumbavu. Sikilizeni maana nitakachosema ni jambo muhimu; midomoni mwangu mtatoka mambo ya adili. Kinywa changu kitatamka kweli tupu; uovu ni chukizo midomoni mwangu. Kinywa changu kitatamka maneno ya kweli, udanganyifu ni haramu midomoni mwangu. Kwa mtu mwelewa kila kitu ni wazi, kwa mwenye maarifa yote ni sawa. Chagua mafundisho yangu badala ya fedha; na maarifa badala ya dhahabu safi. “Mimi Hekima nina thamani kuliko johari; chochote unachotamani hakiwezi kulingana nami.
Methali 8:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu. Sikilizeni, maana nitasema yaliyo mazuri, Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili. Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Yote humwelea yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa. Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi. Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.
Methali 8:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu. Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri, Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili. Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Yote humwelea yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa. Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi. Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.
Methali 8:1-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti? Juu ya miinuko karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo; kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema: “Ni ninyi watu, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote. Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili; ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu. Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema; ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa. Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu. Maneno yote ya kinywa changu ni ya haki; hakuna mojawapo lililopotoka au la ukaidi. Kwa wenye kupambanua, yote ni sahihi; hayana kasoro kwa wale wenye maarifa. Chagua mafundisho yangu badala ya fedha, maarifa badala ya dhahabu safi, kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.