Methali 7:24-27
Methali 7:24-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Sasa wanangu, nisikilizeni; yategeeni sikio maneno ya kinywa changu. Msikubali kuongozwa na mwanamke kama huyo, wala msipitepite katika mapito yake. Maana amewaangusha wanaume wengi; ni wengi mno hao aliowachinja. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, ni mahali pa kuteremkia mautini.
Methali 7:24-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. Maana amewaangusha wengi aliowajeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni wengi. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.
Methali 7:24-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.
Methali 7:24-27 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo. Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake. Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa. Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.