Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 7:14-27 - Compare All Versions

Methali 7:14-27 BHN (Biblia Habari Njema)

“Ilinilazimu kutoa tambiko zangu; leo hii nimekamilisha nadhiri yangu. Ndio maana nimetoka ili nikulaki, nimekutafuta kwa hamu nikakupata. Nimetandika kitanda changu vizuri, kwa shuka za rangi za kitani kutoka Misri. Nimekitia manukato, manemane, udi na mdalasini. Njoo tulale pamoja mpaka asubuhi; njoo tujifurahishe kwa mahaba. Mume wangu hayumo nyumbani, amekwenda safari ya mbali. Amechukua bunda la fedha; hatarejea nyumbani karibuni.” Alimshawishi kwa maneno mengi ya kubembeleza; kijana akashawishika kwa maneno yake matamu. Hapo akamfuata huyo mwanamke moja kwa moja, kama ng'ombe aendaye machinjioni, kama paa arukiaye mtegoni. Hakutambua kwamba hiyo itamgharimu maisha yake, mpaka alipojikuta amekuwa kama amechomwa mshale moyoni, amekuwa kama ndege aliyenaswa wavuni. Sasa wanangu, nisikilizeni; yategeeni sikio maneno ya kinywa changu. Msikubali kuongozwa na mwanamke kama huyo, wala msipitepite katika mapito yake. Maana amewaangusha wanaume wengi; ni wengi mno hao aliowachinja. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, ni mahali pa kuteremkia mautini.

Shirikisha
Methali 7 BHN

Methali 7:14-27 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona. Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari. Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini. Haya, na tushibe upendo hadi asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba. Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali; Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu. Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. Maana amewaangusha wengi aliowajeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni wengi. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.

Shirikisha
Methali 7 SRUV

Methali 7:14-27 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona. Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari. Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini. Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba. Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali; Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu. Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.

Shirikisha
Methali 7 SUV

Methali 7:14-27 NEN (Neno)

“Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu. Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata! Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri. Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini. Njoo, tuzame katika mapenzi hadi asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi! Mume wangu hayupo nyumbani; ameenda safari ya mbali. Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwa nyumbani karibuni.” Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini. Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi, hadi mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo. Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake. Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa. Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.

Shirikisha
Methali 7 NEN