Methali 7:1-13
Methali 7:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, yashike maneno yangu, zihifadhi kwako amri zangu. Zifuate amri zangu nawe utaishi; yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge vidoleni mwako; yaandike moyoni mwako. Iambie Hekima: “Wewe ni dada yangu”, na Busara “Wewe ni rafiki yangu”. Vitakulinda mbali na mwanamke mbaya, vitakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni. Siku moja dirishani mwa nyumba yangu, nilichungulia nje kupitia viunzi vya dirisha, nikawaona vijana wengi wajinga, na mmoja hasa aliyekuwa mpumbavu. Huyo alikuwa akitembea kwenye barabara ile, karibu na kona alikoishi mwanamke fulani. Basi akashika njia iendayo nyumbani kwa mwanamke huyo. Ilikuwa yapata wakati wa jioni, giza na usiku vilikuwa vimeanza kuingia. Punde kijana akakutana na huyo mwanamke; amevalia kama malaya, ana mipango yake. Alikuwa mwanamke wa makelele na mkaidi; miguu yake haitulii nyumbani: Mara barabarani, mara sokoni, katika kila kona ya njia hakosekani akivizia. Alimkumbatia kijana huyo na kumbusu, na kwa maneno matamu, akamwambia
Methali 7:1-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, Wewe ndiwe dada yangu; Mwite ufahamu jamaa yako mwandani. Wapate kukulinda na malaya, Na mwasherati akubembelezaye kwa maneno yake. Maana katika dirisha la nyumba yangu Nilichungulia katika shubaka yake. Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake, Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani. Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake. Mara yuko katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia. Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya
Methali 7:1-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake. Maana katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika shubaka yake; Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake, Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani. Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake. Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia. Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya
Methali 7:1-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako; watakuepusha na mwanamke mzinzi, kutokana na mwanamke mpotovu na maneno yake ya kubembeleza. Kwenye dirisha la nyumba yangu nilitazama nje kupitia upenyo kwenye mwimo wa dirisha. Niliona miongoni mwa wajinga, nikagundua miongoni mwa wanaume vijana, kijana asiye na akili. Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia. Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya hila. (Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani; mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.) Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia