Methali 5:7-14 - Compare All Versions
Methali 5:7-14 BHN (Biblia Habari Njema)
Sasa enyi wanangu, nisikilizeni, wala msisahau maneno ya kinywa changu. Iepushe njia yako mbali naye, wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, na wakatili miaka yako; wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako, na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni. Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Sikuisikiliza sauti ya waalimu wangu, wala kuwategea sikio wakufunzi wangu. Sasa niko karibu kuangamia kabisa mbali na jumuiya ya watu.”
Methali 5:7-14 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.
Methali 5:7-14 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakatili miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.
Methali 5:7-14 NEN (Neno)
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia. Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake, usije ukapoteza heshima yako kwa wengine, na miaka yako kwa aliye mkatili, wageni wasije wakasherehekea utajiri wako, na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine. Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa. Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! Sikuwatii walimu wangu, wala kuwasikiliza wakufunzi wangu. Nimefika ukingoni mwa maangamizi katika kusanyiko la watu wa Mungu.”