Methali 5:7-10
Methali 5:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Sasa enyi wanangu, nisikilizeni, wala msisahau maneno ya kinywa changu. Iepushe njia yako mbali naye, wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, na wakatili miaka yako; wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako, na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni.
Methali 5:7-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakatili miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni
Methali 5:7-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni
Methali 5:7-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia. Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake, usije ukapoteza heshima yako kwa wengine, na miaka yako kwa aliye mkatili, wageni wasije wakasherehekea utajiri wako, na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine.