Methali 5:3-6
Methali 5:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mdomo wa mwanamke mpotovu ni mtamu kama asali, maneno yake ni laini kuliko mafuta; lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Nyayo zake zaelekea chini mautini, hatua zake zaenda kuzimu. Yeye haijali njia ya uhai, njia zake ni za kutangatanga, wala hajui.
Methali 5:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana midomo ya malaya hudondosha asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Miguu yake inateremkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari.
Methali 5:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.
Methali 5:3-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta; lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. Yeye hafikirii kuhusu njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.