Methali 5:1-7
Methali 5:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. Ndipo utakapoweza kuhifadhi busara, na midomo yako izingatie maarifa. Mdomo wa mwanamke mpotovu ni mtamu kama asali, maneno yake ni laini kuliko mafuta; lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Nyayo zake zaelekea chini mautini, hatua zake zaenda kuzimu. Yeye haijali njia ya uhai, njia zake ni za kutangatanga, wala hajui. Sasa enyi wanangu, nisikilizeni, wala msisahau maneno ya kinywa changu.
Methali 5:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, uzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondosha asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Miguu yake inateremkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu.
Methali 5:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu.
Methali 5:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa. Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta; lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. Yeye hafikirii kuhusu njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.