Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 5:1-23

Methali 5:1-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.

Shirikisha
Soma Methali 5

Methali 5:1-23 Biblia Habari Njema (BHN)

Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. Ndipo utakapoweza kuhifadhi busara, na midomo yako izingatie maarifa. Mdomo wa mwanamke mpotovu ni mtamu kama asali, maneno yake ni laini kuliko mafuta; lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Nyayo zake zaelekea chini mautini, hatua zake zaenda kuzimu. Yeye haijali njia ya uhai, njia zake ni za kutangatanga, wala hajui. Sasa enyi wanangu, nisikilizeni, wala msisahau maneno ya kinywa changu. Iepushe njia yako mbali naye, wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, na wakatili miaka yako; wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako, na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni. Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Sikuisikiliza sauti ya waalimu wangu, wala kuwategea sikio wakufunzi wangu. Sasa niko karibu kuangamia kabisa mbali na jumuiya ya watu.” Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe. Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani? Hiyo ni yako wewe mwenyewe, wala usiwashirikishe watu wengine. Chemchemi yako na ibarikiwe, umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana. Ni mzuri kama ayala, apendeza kama paa. Mahaba yake yakufurahishe kila wakati, umezwe daima na pendo lake. Mwanangu, ya nini kutekwa na mwanamke mwasherati? Ya nini kumkumbatia kifuani mwanamke mgeni? Kumbuka njia za mtu zi wazi mbele ya Mwenyezi-Mungu; yeye anaona kila hatua anayochukua binadamu. Mtu mwovu hunaswa kwa uovu wake mwenyewe; hukamatwa katika tanzi za dhambi yake mwenyewe. Yeye hufa kwa utovu wa nidhamu, huangamia kwa sababu ya upuuzi wake mkuu.

Shirikisha
Soma Methali 5

Methali 5:1-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, uzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondosha asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Miguu yake inateremkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakatili miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. Unywe maji ya tangi lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Matiti yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.

Shirikisha
Soma Methali 5

Methali 5:1-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.

Shirikisha
Soma Methali 5

Methali 5:1-23 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa. Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta; lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. Yeye hafikirii kuhusu njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia. Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake, usije ukapoteza heshima yako kwa wengine, na miaka yako kwa aliye mkatili, wageni wasije wakasherehekea utajiri wako, na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine. Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa. Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! Sikuwatii walimu wangu, wala kuwasikiliza wakufunzi wangu. Nimefika ukingoni mwa maangamizi katika kusanyiko la watu wa Mungu.” Kunywa maji kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kisima chako mwenyewe. Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani? Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni. Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako. Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake. Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine? Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za BWANA, naye huyapima mapito yake yote. Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu. Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.

Shirikisha
Soma Methali 5