Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 5:1-19

Methali 5:1-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.

Shirikisha
Soma Methali 5

Methali 5:1-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, uzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondosha asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Miguu yake inateremkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakatili miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. Unywe maji ya tangi lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Matiti yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.

Shirikisha
Soma Methali 5

Methali 5:1-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.

Shirikisha
Soma Methali 5

Methali 5:1-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa. Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta; lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. Yeye hafikirii kuhusu njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia. Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake, usije ukapoteza heshima yako kwa wengine, na miaka yako kwa aliye mkatili, wageni wasije wakasherehekea utajiri wako, na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine. Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa. Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! Sikuwatii walimu wangu, wala kuwasikiliza wakufunzi wangu. Nimefika ukingoni mwa maangamizi katika kusanyiko la watu wa Mungu.” Kunywa maji kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kisima chako mwenyewe. Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani? Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni. Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako. Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.

Shirikisha
Soma Methali 5