Methali 30:7-9
Methali 30:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu, wala usinikatalie kabla sijafa: Uniondolee uongo na udanganyifu; usinipe umaskini wala utajiri; unipatie chakula ninachohitaji, nisije nikashiba nikakukana; nikasema, “Mwenyezi-Mungu ni nani?” Au nisije nikawa maskini nikaiba, na kulikufuru jina lako ee Mungu wangu.

Methali 30:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
Methali 30:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
Methali 30:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Ninakuomba vitu viwili, Ee BWANA; usininyime kabla sijafa: Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘BWANA ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.