Methali 29:24-27
Methali 29:24-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Anayeshirikiana na mwizi anajidhuru mwenyewe; husikia laana ya aliyeonewa bila kusema neno. Kuwaogopa watu ni kujitega mwenyewe, lakini anayemtumaini Mwenyezi-Mungu yu salama. Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala, hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu. Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu, naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu.
Methali 29:24-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mshiriki wa mwizi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Methali 29:24-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mshiriki wa mwivi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Methali 29:24-27 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia. Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye BWANA atakuwa salama. Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa BWANA. Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki.