Methali 29:2-18
Methali 29:2-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Waadilifu wakitawala watu hufurahi, lakini waovu wakitawala watu hulalamika. Apendaye hekima humfurahisha baba yake; lakini aandamanaye na malaya hufuja mali yake. Mfalme akitumia haki huipatia nchi uthabiti, lakini akipenda hongo taifa huangamia. Mwenye kumbembeleza jirani yake, anatega mtego wa kujinasa mwenyewe. Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake, lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi. Mwadilifu anajua haki za maskini, lakini mtu mwovu hajui mambo hayo. Wenye dharau huutia vurugu mji mzima, lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu. Mwenye hekima akibishana na mpumbavu, mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia. Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake. Mpumbavu huonesha hasira yake wazi, lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza. Mtawala akisikiliza mambo ya uongo, maofisa wake wote watakuwa waovu. Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja: Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu. Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele. Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake. Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi; yeye ataufurahisha moyo wako. Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu; heri mtu yule anayeshika sheria.
Methali 29:2-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua. Apendaye hekima humfurahisha babaye; Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali. Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua. Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi. Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini; Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue. Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu. Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha. Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza. Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu. Maskini na mdhalimu hukutana pamoja; BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili. Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele. Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako. Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
Methali 29:2-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Methali 29:2-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake. Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza. Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. Mwovu hutegwa na dhambi yake mwenyewe, bali mwenye haki hushangilia na kufurahi. Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo. Wanaodhihaki huuchochea mji, bali wenye hekima huzuia hasira. Mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu, na hutafuta kumuua mtu mnyofu. Mpumbavu huonesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia. Mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu. Mtu maskini na mtu mdhalimu wanafanana kwa jambo hili: BWANA hutia nuru macho yao wote wawili. Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake kitakuwa thabiti daima. Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake. Waovu wanapostawi, dhambi huongezeka pia; lakini wenye haki wataliona anguko lao. Mkanye mwanao, naye atakupa amani; atakuletea furaha unayotamani. Mahali pasipo na ufunuo, watu huacha kujizuia, bali ana heri mtu yule anayeitii sheria.