Methali 28:7-17
Methali 28:7-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtoto ashikaye sheria ni mwenye hekima, lakini rafiki wa walafi humwaibisha baba yake. Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini. Anayekataa kuisikia sheria, huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu. Anayemshawishi mtu mwema kutenda mabaya, ataanguka katika shimo lake mwenyewe. Wasio na hatia wamewekewa mema yao. Tajiri hujiona mwenyewe kuwa mwenye hekima, lakini maskini mwenye busara atamfichua. Watu wema wakipata madaraka maisha hufana, lakini waovu wakitawala watu hujificha. Afichaye makosa yake hatafanikiwa; lakini anayeungama na kuyaacha atapata rehema. Heri mtu amchaye Mwenyezi-Mungu daima; lakini mkaidi wa moyo ataangukia maafa. Mtawala mwovu anayewatawala maskini, ni kama simba angurumaye au dubu anayeshambulia. Mtawala asiye na akili ni mdhalimu mkatili; lakini achukiaye mali ya udanganyifu atatawala muda mrefu. Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu, atakuwa mkimbizi mpaka kaburini; mtu yeyote na asijaribu kumzuia.
Methali 28:7-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye. Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema. Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe; Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana. Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha. Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara. Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini. Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake. Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.
Methali 28:7-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Methali 28:7-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yeye anayetii sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake. Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini. Mtu yeyote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo. Yeye anayemwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema. Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye busara humtambua alivyodanganyika. Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha. Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha BWANA, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huanguka kwenye taabu. Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, ndivyo alivyo mtu mwovu anayetawala wanyonge. Mtawala dhalimu hana akili, bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu atafurahia maisha marefu. Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro hadi kufa; mtu yeyote asimsaidie.