Methali 28:3-5
Methali 28:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini, amefanana na mvua kubwa inayoharibu mimea. Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu, lakini wanaoishika sheria hupingana nao. Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa.
Methali 28:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula. Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. Watu waovu hawaelewi na haki; Bali wamtafutao BWANA huelewa na zote.
Methali 28:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula. Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote.
Methali 28:3-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mtawala anayewadhulumu maskini, ni kama mvua ya dhoruba inayoharibu mazao yote. Wale wanaoacha sheria huwasifu waovu, bali wale wanaotii sheria huwapinga. Wapotovu hawaelewi haki, bali wale wanaomtafuta BWANA wanaielewa kikamilifu.