Methali 27:7-9
Methali 27:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Aliyeshiba hata asali huikataa, lakini kwa mwenye njaa kila kichungu ni kitamu. Mtu aliyepotea mbali na kwake, ni kama ndege aliyepotea mbali na kiota chake. Mafuta na manukato huufurahisha moyo, lakini taabu hurarua roho.
Methali 27:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu. Kama ndege aendaye huku na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huku na huko mbali na mahali pake. Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.
Methali 27:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu. Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake. Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.
Methali 27:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, bali kwa mwenye njaa hata kile kilicho kichungu kwake ni kitamu. Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake. Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka katika ushauri wake wa uaminifu.