Methali 27:1-4
Methali 27:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Usijisifie ya kesho, hujui nini kitatokea leo mpaka kesho. Acha watu wengine wakusifu, kuliko mdomo wako wewe mwenyewe. Jiwe ni zito na mchanga kadhalika, lakini usumbufu wa mpumbavu ni mzito zaidi. Ghadhabu ni katili na hasira huangamiza; lakini ni nani awezaye kuukabili wivu?
Methali 27:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe. Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili. Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
Methali 27:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe. Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili. Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
Methali 27:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe. Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili. Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?