Methali 24:3-6
Methali 24:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Methali 24:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyumba hujengwa kwa hekima, na kuimarishwa kwa busara. Kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. Kuwa na hekima ni bora kuliko kuwa na nguvu, naam, maarifa ni bora kuliko nguvu. Maana kwa mwongozo mzuri waweza kupigana vita, na kwa washauri wengi ushindi hupatikana.
Methali 24:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Methali 24:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Methali 24:3-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kupitia ufahamu huimarishwa; kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu, kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi.