Methali 24:11-12
Methali 24:11-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Usiseme baadaye: “Hatukujua!” Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona; yeye atakulipa kulingana na matendo yako!
Methali 24:11-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Methali 24:11-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Methali 24:11-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. Mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?