Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 24:1-34

Methali 24:1-34 Biblia Habari Njema (BHN)

Usiwaonee wivu watu waovu, wala usitamani kuwa pamoja nao, maana fikira zao zote ni juu ya ukatili, hamna jema lolote litokalo midomoni mwao. Nyumba hujengwa kwa hekima, na kuimarishwa kwa busara. Kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. Kuwa na hekima ni bora kuliko kuwa na nguvu, naam, maarifa ni bora kuliko nguvu. Maana kwa mwongozo mzuri waweza kupigana vita, na kwa washauri wengi ushindi hupatikana. Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa; penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo. Afikiriaye kutenda maovu daima ataitwa mtu mwenye fitina. Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu. Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli. Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Usiseme baadaye: “Hatukujua!” Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona; yeye atakulipa kulingana na matendo yako! Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni. Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako; ukiipata utakuwa na matazamio mema, wala tumaini lako halitakuwa la bure. Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema, wala usijaribu kuiharibu nyumba yake, maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga. Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake, maana Mwenyezi-Mungu aonaye hayo hatapendezwa; huenda akaacha kumwadhibu. Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, wala usiwaonee wivu watu waovu, maana mwovu hatakuwa na mema baadaye; taa ya uhai wake itazimwa. Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme, wala usishirikiane na wale wasio na msimamo, maana maangamizi yao huwapata ghafla. Hakuna ajuaye maafa watakayozusha. Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima: Kupendelea watu katika hukumu si vizuri. Anayemwachilia mtu mwenye hatia, hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa. Lakini wanaowaadhibu waovu watapata furaha, na baraka njema zitawajia. Jibu lililo la haki, ni kama busu la rafiki. Kwanza fanya kazi zako nje, tayarisha kila kitu shambani, kisha jenga nyumba yako. Usishuhudie bure dhidi ya jirani yako, wala usiseme uongo juu yake. Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda! Ni lazima nilipize kisasi!” Nilipitia karibu na shamba la mvivu; shamba la mzabibu la mtu mpumbavu. Nilishangaa kuona limemea miiba, magugu yamefunika eneo lake lote, na ukuta wake wa mawe umebomoka. Nilitazama, nikawaza, mwishowe nikapata funzo: Lala tu kidogo; sinzia tu kidogo! Kunja mikono yako tu upumzike! Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini, umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara kama mtu mwenye silaha.

Shirikisha
Soma Methali 24

Methali 24:1-34 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Usiwawaonee wivu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao; Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara. Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu. Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni. Mtu afikiriye kutenda maovu, Watu watamwita mtundu; Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu. Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache. Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake? Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika. Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika; Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya. Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake. Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya; Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika. Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu; Maana msiba wao utatokea kwa ghafla; Tena ni nani aujuaye uharibifu wa miaka yao. Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Makabila ya watu watamlaani, taifa watamchukia. Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia. Aibusu midomo atoaye jawabu la haki. Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako. Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako. Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake. Nilipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Niliona, nikapata mafundisho. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Shirikisha
Soma Methali 24

Methali 24:1-34 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Usiwahusudu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao; Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara. Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo; Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu. Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni. Mtu afikiriye kutenda maovu, Watu watamwita mtundu; Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu. Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache. Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake? Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika. Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika; Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya. Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake. Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya; Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika. Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu; Maana msiba wao utatokea kwa ghafula; Tena ni nani aujuaye uharibifu wa miaka yao. Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia. Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia. Aibusu midomo atoaye jawabu la haki. Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako. Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako. Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake. Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Shirikisha
Soma Methali 24

Methali 24:1-34 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao; kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema kuhusu kuleta madhara. Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kupitia ufahamu huimarishwa; kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu, kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi. Hekima i juu mno kwa mpumbavu, katika kusanyiko langoni hana lolote la kusema. Yeye apangaye mabaya atajulikana kama mtu wa hila. Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka. Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo! Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. Mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda? Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka sega ni tamu kwa kuonja. Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako: Ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali. Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake, kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena; lakini waovu huangushwa chini na maafa. Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati anapojikwaa, usiruhusu moyo wako ushangilie. BWANA asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye. Usikasirike kwa sababu ya wapotovu, wala usiwaonee wivu waovu, kwa maana mpotovu hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa. Mwanangu, mche BWANA na mfalme, wala usijiunge na waasi, kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta? Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonesha upendeleo katika hukumu si vyema: Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” makabila ya watu watamlaani, na mataifa watamkana. Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, nazo baraka tele zitawajilia juu yao. Jawabu la uaminifu ni kama busu la mdomoni. Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako. Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya. Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.” Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka. Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona: Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: na umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

Shirikisha
Soma Methali 24