Methali 23:22-25
Methali 23:22-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Msikilize baba yako aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako akizeeka. Nunua ukweli, wala usiuuze; nunua hekima, mafunzo na busara. Baba wa mtoto mwadilifu atajaa furaha; anayemzaa mtoto mwenye hekima atamfurahia. Wafurahishe baba na mama yako; mama aliyekuzaa na afurahi.
Methali 23:22-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee. Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu. Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia. Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa.
Methali 23:22-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee. Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu. Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia. Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa.
Methali 23:22-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Msikilize baba yako, aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee. Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu. Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa, naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia. Baba yako na mama yako na wafurahi, mama aliyekuzaa na ashangilie!