Methali 23:17-21
Methali 23:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Moyo wako usiwaonee wivu wenye dhambi, ila endelea kumcha Mwenyezi-Mungu siku zote. Hakika kuna kesho ya milele, na tumaini lako halitakuwa bure. Sikia mwanangu, uwe na hekima; fikiria sana jinsi unavyoishi. Usiwe mmoja wa walevi wa divai, wala walafi wenye kupenda nyama, maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini, anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara.
Methali 23:17-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa; Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika. Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema. Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Methali 23:17-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa; Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika. Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema. Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Methali 23:17-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha BWANA. Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali. Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima, weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa. Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa, kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara.