Methali 22:17-29
Methali 22:17-29 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako na kuwa nayo yote tayari mdomoni mwako. Ili tumaini lako liwe katika BWANA, hata wewe, ninakufundisha leo. Je, sijakuandikia misemo thelathini, misemo ya mashauri na maarifa, kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika, ili uweze kutoa majibu sahihi kwake yeye aliyekutuma? Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini, wala kumdhulumu mhitaji mahakamani, kwa sababu BWANA atawatetea naye atawateka hao waliowateka. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka, usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika, la sivyo utajifunza njia zake na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego. Usiwe mwenye kupeana mikono katika rehani, au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni; ukikosa njia ya kulipa, kitanda chako kitachukuliwa ukiwa umekilalia. Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani lililowekwa na baba zako. Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake? Atahudumu mbele ya wafalme; hatahudumu mbele ya watu duni.
Methali 22:17-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli? Usimnyang’anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego. Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako? Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako. Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.
Methali 22:17-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli? Usimnyang'anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego. Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako? Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako. Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.
Methali 22:17-29 Biblia Habari Njema (BHN)
Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima, elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu. Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni, na kuyakariri kila wakati. Ninayependa kumfundisha leo ni wewe, ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu. Nimekuandikia misemo thelathini, misemo ya maonyo na maarifa, ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli; na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi. Usimdhulumu maskini kwa kuwa ni maskini, wala usimnyime fukara haki yake mahakamani. Maana Mwenyezi-Mungu atawatetea; atawapokonya maisha yao wale watakaowadhulumu. Usifanye urafiki na mtu wa hasira, wala usiandamane na mwenye ghadhabu, usije ukajifunza mwenendo wake, ukajinasa kabisa katika mtego. Usiwe mmoja wao wenye kuweka ahadi, watu ambao hujiweka wadhamini wa madeni. Ikiwa huna chochote cha kulipa, hata kitanda unacholalia kitachukuliwa! Usiondoe alama ya mipaka ya zamani ambayo iliwekwa na wazee wako. Je, yuko mtu mwenye maarifa kazini mwake? Huyo atawatumikia wafalme; hatawapa huduma yake watu wasiofaa.