Methali 22:10-12
Methali 22:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka, ugomvi na matusi vitakoma. Mwenye nia safi na maneno mazuri, atakuwa rafiki wa mfalme. Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli, lakini huyavuruga maneno ya waovu.
Methali 22:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma. Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini.
Methali 22:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma. Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini.
Methali 22:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mfukuze mwenye dhihaka, na mvutano utatoweka; ugomvi na matukano vitakoma. Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.