Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 22:1-29

Methali 22:1-29 Biblia Habari Njema (BHN)

Afadhali kuwa na sifa nzuri kuliko mali nyingi; wema ni bora kuliko fedha au dhahabu. Matajiri na maskini wana hali hii moja: Mwenyezi-Mungu ni Muumba wao wote. Mtu mwangalifu huona hatari akajificha, lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia. Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu, utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai. Njia ya waovu imejaa miiba na mitego; anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa. Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni. Tajiri humtawala maskini; mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji. Apandaye dhuluma atavuna janga; uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa. Mtu mkarimu atabarikiwa, maana chakula chake humgawia maskini. Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka, ugomvi na matusi vitakoma. Mwenye nia safi na maneno mazuri, atakuwa rafiki wa mfalme. Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli, lakini huyavuruga maneno ya waovu. Mvivu husema, “Siwezi kutoka nje; kuna simba huko, ataniua!” Kinywa cha mwasherati ni shimo refu; anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo. Mtoto hupenda mambo ya kijinga moyoni, lakini fimbo ya nidhamu humwondolea hayo. Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe, anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini. Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima, elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu. Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni, na kuyakariri kila wakati. Ninayependa kumfundisha leo ni wewe, ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu. Nimekuandikia misemo thelathini, misemo ya maonyo na maarifa, ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli; na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi. Usimdhulumu maskini kwa kuwa ni maskini, wala usimnyime fukara haki yake mahakamani. Maana Mwenyezi-Mungu atawatetea; atawapokonya maisha yao wale watakaowadhulumu. Usifanye urafiki na mtu wa hasira, wala usiandamane na mwenye ghadhabu, usije ukajifunza mwenendo wake, ukajinasa kabisa katika mtego. Usiwe mmoja wao wenye kuweka ahadi, watu ambao hujiweka wadhamini wa madeni. Ikiwa huna chochote cha kulipa, hata kitanda unacholalia kitachukuliwa! Usiondoe alama ya mipaka ya zamani ambayo iliwekwa na wazee wako. Je, yuko mtu mwenye maarifa kazini mwake? Huyo atawatumikia wafalme; hatawapa huduma yake watu wasiofaa.

Shirikisha
Soma Methali 22

Methali 22:1-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. Tajiri na maskini hukutana pamoja; BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili. Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima. Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo. Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye. Yeye apandaye uovu atavuna msiba, Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma. Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake. Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma. Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini. Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu. Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake. Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali. Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara. Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli? Usimnyang'anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego. Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako? Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako. Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.

Shirikisha
Soma Methali 22

Methali 22:1-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. Tajiri na maskini hukutana pamoja; BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili. Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima. Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo. Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye. Yeye apandaye uovu atavuna msiba, Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma. Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake. Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma. Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini. Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu. Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake. Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali. Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara. Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli? Usimnyang’anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego. Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako? Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako. Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.

Shirikisha
Soma Methali 22

Methali 22:1-29 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi; kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu. Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: BWANA ni Muumba wao wote. Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara. Unyenyekevu na kumcha BWANA huleta utajiri, heshima na uzima. Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego, bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo. Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee. Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye. Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa. Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini. Mfukuze mwenye dhihaka, na mvutano utatoweka; ugomvi na matukano vitakoma. Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu. Mvivu husema, “Yuko simba nje!” au, “Nitauawa katika mitaa!” Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu; yeye aliye chini ya ghadhabu ya BWANA atatumbukia ndani yake. Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye. Yeye anayemdhulumu maskini ili kujiongezea mali, naye anayempa tajiri zawadi, wote huwa maskini. Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako na kuwa nayo yote tayari mdomoni mwako. Ili tumaini lako liwe katika BWANA, hata wewe, ninakufundisha leo. Je, sijakuandikia misemo thelathini, misemo ya mashauri na maarifa, kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika, ili uweze kutoa majibu sahihi kwake yeye aliyekutuma? Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini, wala kumdhulumu mhitaji mahakamani, kwa sababu BWANA atawatetea naye atawateka hao waliowateka. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka, usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika, la sivyo utajifunza njia zake na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego. Usiwe mwenye kupeana mikono katika rehani, au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni; ukikosa njia ya kulipa, kitanda chako kitachukuliwa ukiwa umekilalia. Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani lililowekwa na baba zako. Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake? Atahudumu mbele ya wafalme; hatahudumu mbele ya watu duni.

Shirikisha
Soma Methali 22