Methali 21:5-7
Methali 21:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mipango ya mtu wa bidii huleta mali kwa wingi, lakini kila aliye na pupa huishia patupu. Mali ipatikanayo kwa udanganyifu, ni mvuke upitao na mtego wa kifo. Ukatili wa wakatili utawafutilia mbali, maana wanakataa kutenda yaliyo ya haki.
Methali 21:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji. Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti. Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali; Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu.
Methali 21:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji. Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti. Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali; Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu.
Methali 21:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini. Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha. Jeuri ya waovu itawaburuta mbali, kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa.