Methali 21:5-16
Methali 21:5-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Mipango ya mtu wa bidii huleta mali kwa wingi, lakini kila aliye na pupa huishia patupu. Mali ipatikanayo kwa udanganyifu, ni mvuke upitao na mtego wa kifo. Ukatili wa wakatili utawafutilia mbali, maana wanakataa kutenda yaliyo ya haki. Njia ya mtu mwenye hatia imepotoka, lakini mwenendo wa mnyofu umenyooka. Afadhali kuishi pembeni juu ya paa, kuliko kuishi nyumbani na mwanamke mgomvi. Anachopania kutenda mtu mbaya ni uovu; hata kwa jirani yake hana huruma. Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima; ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa. Mungu Mwadilifu anajua wanayotenda waovu nyumbani kwao; naye atawaangusha na kuwaangamiza. Anayekataa kusikiliza kilio cha maskini, naye pia hatasikilizwa atakapolilia msaada. Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri; tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu. Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa. Anayetangatanga mbali na njia ya busara, atajikuta ametua miongoni mwa wafu.
Methali 21:5-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji. Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti. Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali; Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu. Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana; Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi. Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu; Jirani yake hapati fadhili machoni pake. Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima; Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa. Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya; Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia. Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa. Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali. Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu; Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu. Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa.
Methali 21:5-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Methali 21:5-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini. Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha. Jeuri ya waovu itawaburuta mbali, kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa. Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu, bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu. Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake. Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, mjinga hupata hekima; wakati mtu mwenye hekima anafundishwa, hupata maarifa. Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu, naye atawaangamiza waovu. Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini, yeye pia atalia, wala hatajibiwa. Zawadi inayotolewa kwa siri hutuliza hasira, na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali hofu kwa watenda maovu. Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa.