Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 19:1-29

Methali 19:1-29 Biblia Habari Njema (BHN)

Afadhali maskini aishiye kwa unyofu, kuliko mtu mpotovu wa maneno na mpumbavu. Haifai mtu kuwa bila akili; mwenda harakaharaka hujikwaa. Mtu akijiangamiza kwa upumbavu wake, huielekeza hasira yake dhidi ya Mwenyezi-Mungu. Mali huvuta marafiki wengi wapya, lakini maskini huachwa bila rafiki. Shahidi mwongo hataacha kuadhibiwa; asemaye uongo hataepa adhabu. Watu wengi hujipendekeza kwa wakuu; kila mtu hutaka kuwa rafiki ya mtu mkarimu. Maskini huchukiwa na ndugu zake; marafiki zake ndio zaidi: Humkimbia! Hata awabembeleze namna gani hatawapata. Ajipatiaye hekima anaipenda nafsi yake; anayezingatia busara atastawi. Shahidi mwongo hatakosa kuadhibiwa; asemaye uongo ataangamia. Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa, tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu. Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari kwake. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba, lakini wema wake ni kama umande juu ya majani. Mtoto mpumbavu ni balaa kwa baba yake; na ugomvi wa mke ni kama matone ya mvua yasiyoisha. Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa wazee wake, lakini mke mwenye busara hutoka kwa Mwenyezi-Mungu. Uzembe ni kama usingizi mzito; mtu mvivu atateseka kwa njaa. Anayeshika amri anasalimisha maisha yake; anayepuuza agizo atakufa. Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema. Mrudi mwanao kungali bado na tumaini, lakini usimwadhibu kiasi cha kumwangamiza. Mtu wa hasira kali lazima apate adhabu; ukimwachia mara moja itakubidi kumwachia tena. Sikiliza shauri na kupokea mafundisho, upate hekima ya kukufaa siku zijazo. Kichwani mwa mtu mna mipango mingi, lakini anachokusudia Mwenyezi-Mungu ndicho kitakachofanyika. Kinachotakiwa kwa mtu ni uaminifu; afadhali mtu maskini kuliko mtu mwongo. Kumcha Mwenyezi-Mungu kunaleta uhai; amchaye hujaliwa pumziko la kutosheleza, wala hatapatwa na baa lolote. Mvivu ni kama mtu atiaye mkono katika sahani ya chakula, lakini hana nguvu ya kuuinua hadi mdomoni. Mwadhibu mwenye mzaha naye mjinga atapata akili; mwonye mwenye busara naye atapata maarifa. Anayemdhulumu baba yake na kumfukuza mama yake, ni mtoto asiyefaa na mpotovu. Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utapotea mara mbali na maneno ya hekima. Shahidi asiyefaa kitu huidhihaki haki; na kinywa cha mwovu hubugia uovu. Adhabu iko tayari kwa wenye mzaha, mijeledi imetayarishwa kuchapa migongo ya wapumbavu.

Shirikisha
Soma Methali 19

Methali 19:1-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Afadhali maskini aendaye katika uadilifu wake, Kuliko mpotovu wa midomo aliye mpumbavu. Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi. Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA. Utajiri huongeza marafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka. Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye zawadi. Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka. Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Naye asemaye uongo ataangamia. Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani. Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke kama kudondoka kwa matone daima. Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA. Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa. Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa. Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema. Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake. Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake, Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena. Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho. Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama. Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo. Kumcha BWANA huelekea uhai; Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya. Mtu mvivu hutia mkono wake katika sahani; Wala hataki hata kuupeleka kinywani pake. Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara; Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa. Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye, Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama. Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa. Shahidi asiyefaa kitu hudhihaki hukumu, Na vinywa vya wasio haki humeza uovu. Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu.

Shirikisha
Soma Methali 19

Methali 19:1-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa midomo aliye mpumbavu. Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi. Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA. Utajiri huongeza rafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka. Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye tunu. Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka. Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Naye asemaye uongo ataangamia. Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani. Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima. Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA. Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa. Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa. Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema. Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake. Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake, Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena. Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho. Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama. Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo. Kumcha BWANA huelekea uhai; Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake. Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara; Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa. Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye, Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama. Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa. Shahidi asiyefaa kitu hudhihaki hukumu, Na vinywa vya wasio haki humeza uovu. Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu.

Shirikisha
Soma Methali 19

Methali 19:1-29 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia. Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake hata hivyo moyo wake humkasirikia BWANA. Mali huleta rafiki wengi, bali rafiki wa mtu maskini humwacha. Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru. Wengi hujipendekeza kwa mtawala na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi. Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote: Je, rafiki zake watamkwepa kiasi gani! Ingawa huwafuata kwa kuwasihi, hawapatikani popote. Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi. Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo ataangamia. Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi. Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha. Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa BWANA. Uvivu huleta usingizi mzito, naye mtu mzembe huona njaa. Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake, bali yeye anayezidharau njia zake atakufa. Yeye amhurumiaye maskini humkopesha BWANA, naye atamtuza kwa aliyotenda. Mkanye mwanao, kwa maana kufanya hivyo kuna tumaini, usiwe mshirika katika mauti yake. Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake, kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena. Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho, nawe mwishoni utakuwa na hekima. Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu, lakini kusudi la BWANA ndilo litakalosimama. Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho, afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo. Kumcha BWANA huongoza kwenye uzima, kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, bila kuguswa na shida. Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake! Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara, mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa. Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake ni mwana aletaye aibu na fedheha. Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utatangatanga mbali na maneno ya maarifa. Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi. Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.

Shirikisha
Soma Methali 19