Methali 17:17-19
Methali 17:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote, ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu. Si jambo la akili kuweka rehani, na kuwa mdhamini wa mtu mwingine. Anayependa ugomvi anapenda dhambi; anayejigamba anajitafutia maangamizi.
Methali 17:17-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu. Asiye na hekima hupeana mkono na mtu; Na kuwa mdhamini wa mtu mwingine. Apendaye ugomvi hupenda dhambi; Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.
Methali 17:17-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu. Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu; Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake. Apendaye ugomvi hupenda dhambi; Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.
Methali 17:17-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida. Mtu mjinga huutoa mkono ili kuweka rehani, naye huweka dhamana kwa jirani yake. Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu.