Methali 17:1-4
Methali 17:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Afadhali mkate mkavu kwa amani, kuliko karamu katika nyumba ya ugomvi. Mtumwa mwenye busara atachukua nafasi ya mwana mpumbavu, atapata sehemu ya urithi wa jamaa hiyo. Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu. Mtenda maovu husikiliza maneno mabaya, mwongo hutegea sikio ulimi mdanganyifu.
Methali 17:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi. Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu. Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo. Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu; Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
Methali 17:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi. Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu. Kalibuni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo. Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu; Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
Methali 17:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi. Mtumishi mwenye hekima atamtawala mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu. Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali BWANA huujaribu moyo. Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.