Methali 15:26-30
Methali 15:26-30 Biblia Habari Njema (BHN)
Mawazo ya mwovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, bali maneno mema humfurahisha. Anayetamani faida ya ulanguzi anaitaabisha jamaa yake, lakini achukiaye hongo ataishi. Moyo wa mwadilifu hufikiri kabla ya kujibu, lakini kinywa cha mwovu hububujika uovu. Mwenyezi-Mungu yuko mbali na watu waovu, lakini yu karibu na watu wema kuwasikiliza. Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari njema huuburudisha mwili.
Methali 15:26-30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ushauri mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi. Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi. Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya. BWANA yuko mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki. Mng'ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa.
Methali 15:26-30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mashauri mabaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi. Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi. Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya. BWANA yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki. Mng’ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa.
Methali 15:26-30 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi. Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya. BWANA yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki. Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, nazo habari njema huipa mifupa afya.